• Landtech ltd

  Solutions for land

 • CONTACT US FOR SERVICES

  IBS Cares for you.

 • MATERUNI BLOG FOR MORE NEWS

  WE ARE HERE TO INFORM YOU

 • MUSICS

  MATERUNI NDANI YA BURUDANI.

Friday, 3 July 2015

HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo hadi Jumatatu ya Julai 6, mwaka huu saa 7 mchana.
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya mmoja wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo kuwa mgonjwa na kwa ushauri wa daktari ni kwamba anahitaji mapumziko. Hivyo hukumu hiyo itasomwa Jumatatu ijayo.
Akitoa taarifa hiyo, Hakimu Saul Kinemela ambaye ni mmoja wa jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, amesema mwenyekiti wa jopo lao ambaye ni Jaji John Utamwa ni mgonjwa na kwa ushauri wa daktari hasingeweza kuhudhuria mahakamani hapo. 
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7.

Monday, 29 June 2015

WAUZA MBAO HARAMU WAONYWA

Posted by E.M.OSAKI 18:26


Serikali za Tanzania na Zambia leo zimesaini makubaliano yatakayoziwezesha nchi hizo kuzuia biashara haramu ya mbao na mazao ya misitu, inayovunwa kimagendo katika misitu iliyo mpakani mwa nchi hizo mbili.

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, mheshimiwa Lazaro Nyalandu, amesaini makubaliano hayo kwa niaba ya Tanzania wakati kwa upande wa Zambia, makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa ardhi, maliasili na ulinzi wa mazingira wa nchi hiyo Bi. Christabel Ngimbu.

Waziri Nyalandu amesema kuwa makubaliano hayo yatatoa fursa ya ulinzi na uvunaji sahihi wa maliasili za misitu, hususani miti ya miombo ambayo imekuwa ikitumiwa kwa mbao ambazo majangili huzivuna kiholela kutokana na mwanya wa ukosefu wa ulinzi wa uhakika katika eneo hilo..

UGIRIKI KUFUNGA BENKI KWA WIKI NZIMA

Posted by E.M.OSAKI 18:25
Serikali ya Ugiriki imethibitisha kuwa benki zitafungwa kwa wiki nzima, kufuatia uamuzi uliofanywa na Benki Kuu ya Ulaya wa kuamua kutoendelea kutoa fedha za dharura kwa nchi hiyo.

Katika uamuzi huo wa kisheria ambao ni muhimu katika kulinda mfumo wa fedha wa Ugiriki, kiasi cha mtu kuchukua fedha katika akaunti kimewekewa ukomo kuwa ni dola 66 kwa siku kwa kipindi hiki.

Ugiriki inatarajia kulipa deni la euro bilioni 1.6 kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF) siku ya jumanne, siku ambayo ni ya mwisho ua mpango wa kupatiwa fedha za kuikomboa katika mgogoro wa uchumi itakuwa inaisha.

UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

Posted by E.M.OSAKI 18:24
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imesema kumekuwa na kiwango kikubwa cha ukiukwaji wa haki ya kuwapa chakula watoto wanaotumikia vifungo magerezaji pamoja na wenye umri chini ya miaka mitano katika jamii za wafugaji kutokana na uelewa duni.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Afisa Dawati la Watoto wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Fides Shao amesema watoto walio magerezani wanachanganywa na wakubwa na hivyo kukosa haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na ya kupata chakula, na kwa upande wa jamii za wafugaji kutokana na kuhama kutafuta malisho ya mifugo

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ua Afya na Ustawi wa Jamii katika kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto, Uniti ya Jinsia na Haki za Binadamu, Bi. Notgera Ngaponda amesema wizara imekuwa ikitoa elimu kwa wahudumu wa afya ili kuondokana na unyanyasaji kwa watoto .
Serikali ya Tanzania imetoa onyo kwa wamiliki wa vituo vya mafuta na wasambazaji wa mafuta watakaobainika kuficha bidhaa hiyo na kusema kuwa itawafungia na kuwanyang'anya leseni za umiliki wa biashara ya mafuta.

Akitoa onyo hilo leo bungeni Mjini Dodoma Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa pia serikali itafuatilia aliyesambaza ujumbe wa kuwa kutakua na upungufu wa mafuta kwa siku mbili nchini Tanzania.

Mhe. Mwijage amesema kuwa Serikali inajua takwimu za mafuta yaliyopo ambapo amesema mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya upungufu huo wa mafuta ingawa serikali inafuatilia kwa ukaribu juu ya suala hilo.

 • RSS
 • Delicious
 • Digg
 • Facebook
 • Twitter
 • Linkedin
 • Youtube
 • CONTACT FORM

  Name

  Email *

  Message *

  Blogroll


 • FOLLOWERS

 • VISITORS

  Free HTML Hit Counter

  About

  ON FACEBOOK